19 Machi 2011 - 20:30

Msemaji wa jeshi la Kenya amesema kwamba, ndege za nchi hiyo zimeshambulia kambi moja huko kusini mwa Somalia na kuua wanamgambo 50 wa ash Shabab na kuwajeruhi wengine 60.

Emmanuel Chirchir amesema, wanamgambo hao wa ash Shabab walikuwa katika kambi ya Garbahare na walikuwa wamepanga kushambulia vikosi vya Kenya na vikosi vya serikali ya Somalia katika miji miwili iliyotekwa na wanajeshi wa Kenya wiki hii.Chirchir ameongeza kwamba, hilo ni pigo kubwa kwa wanamgambo hao ambao walipanga kushambulia vikosi vya Kenya katika miji ya Fafadun na Elade.Kenya iliingiza vikosi vyake katika nchi jirani ya Somalia mwezi Oktoba uliopita ili kupambana na wanamgambo wa ash Shabab baada ya wanamgambo hao kushambulia maeneo ya mpakani mwa Kenya na kuteka nyara raia wa kigeni suala ambalo lilitishia sekta ya utalii ya Kenya.